Writen by
sadataley
7:43 AM
-
0
Comments
Gazeti la kila wiki la New York Times, sambamba na kuashiria kesi za ufisadi za baadhi ya viongozi wa Marekani, limeitaja serikali ya Rais Donald Trump kuwa ya kifisadi zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa rais mwaka jana, Trump aliitaja ndege yake binafsi ya Boing 757 kuwa ni 'Alama ya Ustawi wa Biashara ya Trump' suala ambalo liliibua kashafa dhidi ya baadhi ya mawaziri wa serikali yake kama vile Tom Price, Waziri wa Afya na Huduma za Binaadamu na Steven Terner Mnuchin, Waziri wa Hazina na Scott Pruitt, Mkuu wa Taasisi ya Mazingira nchini humo. New York Times pia imeendelea kuibua ufisadi mwingine wa kifedha unaohusishwa na viongozi wa serikali ya Marekani na kusema kuwa, ufisadi ndani ya serikali umeshtadi na kumsahaulisha Trump asiweze hata kukumbuka wadhifa wake.
Gazeti hilo limesisitiza kuwa, ni suala lisilowezekana kumgharamia mara 24 kwa safari za ndege ya binafsi mtu kama Tom Price na kisha kudai kuwa safari hizo zilikuwa ni kwa ajili ya huduma za kijamii kwa kuwa safari hizo pekee ziligharimu kiasi cha dola laki tatu ambazo wamebebeshwa raia wa Marekani kuzilipa. Likiendelea gazeti hilo limeandika kuwa, kukithiri ufisadi ndani ya serikali ya Rais Donald Trump, si jambo ja kushangaza, kwa kuwa mtu huyo haheshimu taasisi yoyote ile ndani ya nchi hiyo.
Parstoday
No comments
Post a Comment