Thursday, September 14, 2017

TFF yagawa mipira 300 kwa vituo vya kukuzia soka la vijana Jijini Dar Es Salaam

 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa mipira 300 kwa viongozi wa vituo na wilaya katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mpango wa kuinua soka la vijana.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda ya Dar es Salaam na makamu mwenyekiti wa soka la Vijana Lameck Nyambaya amekabidhi mipira hiyo kwa lengo la vituo vinavyopatikana jiji la Dar es Saaalm kuweza kuwasaidia na pia kuona soka la vijana linafanikiwa.

Nyambaya alisema TFF watahakikisha mipira hiyo inatumika vizuri ili kutimiza lengo la kuibua na kuwa na vipaji vingi vya mpira ambavyo watakuja kuwa msaada kwa timu za vijana na timu ya taifa.
"Tunaigawa mipira hii kwa vituo vya soka na mimi binafsi nitahakikisha kunakuwa na matumizi sahihi na sio vinginevyo.

Kutokana na ukubwa wa jijini hili, nilimuomba Rais wa TFF atupatie mipira 200 ambayo ametupatia na mimi mwenyewe nitaongeza mipira 100," alisema Nyambaya.

Hivi karibuni, TFF ilianzisha kampeni ya kugawa jumla ya mipira 3,100 ya soka nchi nzima kwa ajili ya soka la vijana.

Mipira hiyo imekabidhiwa kwa viongozi wa wilaya za Kinondoni, Ilala, Temeke, Kigamboni na Ubungo.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment