Thursday, September 28, 2017

Wasiwasi wa kutokuwepo uhuru wa kujieleza katika vyuo vikuu vya Marekani

Mwanasheria Mkuu wa Marekni amekiri kwamba, hakuna uhuru wa kujieleza katika vyuo vikuu vya nchi hiyo.
Jeff Sessions ambaye alikuwa akihutubia hadhaa ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha George Town mjini Washington DC amekosoa suala la kutokuwepo uhuru wa fikra na kujieleza katika vyuo ikuu vya Marekani na kusema kuwa: Kipindi fulani chuo kikuu nhini Marekani kilikuwa kituo cha uhuru na mijadala na sehemu ya ushindani wa fikra na mitazamo mbalimbali lakini sasa vyuo hiyo vimebadilika na kuwa vyumba na kumbi za kuakisi fikra za aina moja za kisiasa. Mwanasheria Mkuu wa Marekani ameongeza kuwa, uhuru wa fikra na uhuru wa kujieleza katika vyuo vikuu unahujumiwa na kushambuliwa na kwamba, baadhi ya vituo vya vyuo vikuu vimeufunga kabisa uhuru.
Maandamano ya kipinga ukatili wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi
Matamshi hayo yametolewa huku baadhi ya wanafunzi wa yuo vikuu waliokuwa wakisikiliza hotuba ya Jeff Sessions wakiwa wameziba midomo yao kwa vitamba kulalamikia suala la kutokuwepo uhuru wa kujieleza katika vyuo vikuu vya Marekani. 
Wanafunzi hao pia walibeba mabango yenye maandishi: "Haki zote za kikatiba na haki za binadamu nchini Marekani zinakabiliwa na hatari.”
Inatupasa kusema hapa kuwa, shughuli za kisiasa hazijafungwa wala kuzuiliwa katika vyuo vikuu vya Marekani na wanafunzi hawazuiwi kuendesha shughuli zao maadamu zinaoana na anga ya kisiasa inayotawala nchi hiyo. Kwa mfano, wafuasi wa vyama viwili vikuu vinavyohodhi siasa za Marekani hawana pingamizi la kujadili kwa kiasi fulani hali ya sasa ya nchi hiyo lakini tatizo linajitokeza pale wanafunzi wa vyuo vikuu wanapotaka kuhoji au kutoa changamoto kwa mfumo wa kisiasa wa Marekani au kukosoa ufisadi wa kisiasa unaofanyika kwa mpangilio maalumu au kupinga dhulma na ukosefu wa usawa na uadilifu wa kijamii na sera za kijeshi na kipolisi zinazogubika jamii ya nchi hiyo. Hali hiyo imeshadidi zaidi baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 kwa kadiri kwamba, woga wa kubambikiziwa tuhuma za ugaidi unawazuia wanafunzi wengi wa vyuo vikuu na wanaharakati wa Marekani kukosoa vikali mipango na harakati za eti kupambana na ugaidi za serikali ya nchi hiyo.
Hii ni katika hali ambayo, maafisa wa vyuo vikuu nchini Marekani wanafanya mikakati ya kuzuia wimbi la harakati za kijamii za kupigania usawa na kupinga ubaguzi wa rangi kama ile ya “Black Lives Matter”, Occupy Wall Street” na ile ya "Tea Party" katika mazingira ya vyuo vikuu.
Yumkini uhuru wa kujieleza kati ya wanavyuo wa Marekani ukawa mkubwa katika vyuo vikuu vya Marekani ikilinganishwa na nchi nyingine duniani, hata hivyo na kwa  mujibu wa matamshi ya  Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Jeff Session, vyuo vikuu vya nchi hiyo vimo katika hali ya kubadilika na kuwa vyumba vilivyofungwa vinavyoakisi fikra za aina moja za kisiasa, suala ambalo linakwamisha hakati za wanavyuo za kutaka kufanyika mabadiliko au mageuzi katika jamii ya nchi hiyo.      
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment