Tuesday, October 3, 2017

Wanawake 100: Je wanawake wanaweza kubadili ulimwengu kwa wiki moja?

Rais Sirleaf Johnson, ,mwanaanga Peggy Whitson na mcheza soka wa Uingereza Steph Houghton.

Haki miliki ya pichaISTOCK
Image captionRais Sirleaf Johnson, ,mwanaanga Peggy Whitson na mcheza soka wa Uingereza Steph Houghton.
Wanawake hawa ni miongoni mwa wale 100 walioteuliwa na BBC kote duniani kwa mchango wao katika maswala ya ya kulinda na kupigania haki za wanawake .
Adele Onyango ni mtangazaji wa redio nchini Kenya
Image captionAdele Onyango ni mtangazaji wa redio nchini Kenya
  • 1.Adelle Onyango
Adele Onyango ni mtangazaji wa redio nchini Kenya anasema kuwa wanawake wa Afrika kwa jumla wanapaswa kujua kwamba ni sawa kuwa vile walivyo , kuona vili walivyo kama uwezo na kuwa huru dhidi ya hofu na ukimya. Adele anapenda kuwawezesha vijana wa kike kupitia ushauri na kuwafunza
  • 2.Anita Nderitu
Ana umri wa miaka 27, na ni mtangazaji wa runinga na habari katika idhaa ya Capital fm. Anasema ''Wanapokwenda chini tunapanda''-Michelle Obama. Bi Nderitu anapenda kuwashauri vijana.
Bi Mwaura ni mwanzilishi wa Flone initiative na afisa wa mawasiliano ITDP Afrika nchini Kenya
Image captionBi Mwaura ni mwanzilishi wa Flone initiative na afisa wa mawasiliano ITDP Afrika nchini Kenya
  • 3.Naomi Mwaura
Bi Mwaura ni mwanzilishi wa Flone initiative na afisa wa mawasiliano ITDP Afrika nchini Kenya. Anasema kuwa wanawake wanahitaji njia nzuri ya kuishi duniani bila ya hofu ya ghasia. Tunafaa kuwa na uwezo wa kuwa mtu yeyote yule. Akiwa Mwanaharakati Naomi alikuwa mmojawapo ya waandalizi dhidi ya unyanyasaji #MyDressMyChoice ambayo ilibadilisha sheria ya unyanyasaji nchini Kenya.
Rais wa Liberia Sirleaf Johnson
Image captionRais wa Liberia Sirleaf Johnson
  • 4.Ellen Sirleaf Johnson
Ana miaka 78 na ni rais wa Liberia. Anasema kuwa ''iwapo ndoto zako hazikugutushi basi ujue sio kubwa''.Ellen ni rais sasa wa Liberia tangu 2006 na rais wa kwanza mwanamke nchini Afrika.
Talent Jumo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Zimbabwe ni mwazilishi na mkurugenzi wa shirika la Katswe Sistahood
Image captionTalent Jumo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Zimbabwe ni mwazilishi na mkurugenzi wa shirika la Katswe Sistahood
  • 5.Talent Jumo
Talent Jumo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Zimbabwe ni mwazilishi na mkurugenzi wa shirika la Katswe Sistahood .
Anasema kuwa siko huru wakati kila mwanamke hayupo huru. Hataiwapo matatizo yake ni tofauti na yangu. Mwanaharakti huyo wa Zimbabwe huwasaidia waathiriwa wa ngono ya kulipza kisasi akiwapatia ushauri nasaha pamoja na ule wa kisheria mbali na kupigania haki za wanawake wanaonyanyaswa kingono na kutoa elimu ya uzazi miongoni mwa wanawake wa Zimbabwe.
Chaima Lasini ni Mwanahabari nchini Morocco
Image captionChaima Lasini ni Mwanahabari nchini Morocco
  • 6.Chaima Lasini
Ni Mwanahabari nchini Morocco .Nimejifunza kwamba watu husahau unachosema, watu watasahau ulichofanya, lakini watu hawatasahau ulivyowafanya kuhisi-Maya Angelou. Chiama ni mwanaharakati wa haki za kike, mwanaharakati wa haki za kibinaadamu na mwandishi kutoka mji mkuu wa Rabat ambaye aliongoza maandamano kufuatia unyanyasaji wa msichana mmoja nchini humo
Mariame Jamme ni mwanzilishi wa shirika la iamth Senegal
Image captionMariame Jamme ni mwanzilishi wa shirika la iamth Senegal
  • 7. Mariame Jamme
Ni mwanzilishi wa shirika la iamth Senegal. Elimu ndio funguo ya dunia na pasipoti ya kujipatia uhuru-Oprah Winfrey. Mfanyibiashara huyu na mwanaharakati alijifunza kusoma na kuandika akiwa na umri wa miaka 16 na sasa ni mfanyibiashara wa kibinafsi.
Nawaal Akram ni mwanamitindo, mcheshi na mwanzilishi wa Muscular Dystrophy nchini Qatar.
Image captionNawaal Akram ni mwanamitindo, mcheshi na mwanzilishi wa Muscular Dystrophy nchini Qatar.
  • 8. Nawaal Akram
Ni mwanamitindo, mcheshi na mwanzilishi wa Muscular Dystrophy nchini Qatar. Kwa kawaida huwa na mwangaza mchache katika giza. Nawaal ni mwanaharakati wa watu walemavu na anapigania haki za wanawake walio na ulemavu mashariki ya kati.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment