Writen by
sadataley
5:09 PM
-
0
Comments
Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,
wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili
ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika
gazeti la Mwananchi.
Mchungaji Kurwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani.
“Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?” alisema Mchungajia Kurwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.
Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari. Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.
Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi. Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.
Na Dotto Mwaibale

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza
lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi
Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani
Kilimanjaro kwa mazishi.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mchungaji Kurwa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, akiongoza ibada hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo akizungumza. Lyimo na marehemu Mmasi wanatoka kijiji kimoja.
Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.
Rafiki wa marehemu Mashaka Mgeta, akizungumzia maisha ya Joyce na jinsi alivyomfahamu.
Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.
Mwanahabari Hellen Mwango akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu.
Mtoto mkubwa wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella, akisoma Historia ya mama yake.
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Thomson, akizungumza katika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.
Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho
Habari kwa Hisani ya Mjengwa Blog
No comments
Post a Comment