Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh William Lukuvu,ametoa siku 30 kwa uongozi wa halmashauri ya Serengeti mkoani Mara kuchukua hatua ya kukabidhi hati 370 za kimila kwa wananchi ambao tayari mashamba yao yamepimwa,lakini wameshindwa kukabidhiwa hati hizo kwa madai ya kukosa picha.
Akizungumza na viongozi wa wilaya ya Serengeti,waziri huyo wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu,ameonesha kusikitishwa baada ya kupata taarifa kuwa wananchi hao 370 tayari mashamba yao yamepangwa na kupimwa,lakini hadi sasa wameshindwa kupatiwa hati hizo kwa kisingizio cha ukosefu wa picha.
Kuhusu wananchi ambao tayari wamejenga nyumba bila ya maeneo hayo kupimwa, waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi,ameagiza mamlaka ya serikali za mitaa kuacha mara moja kuvunja nyumba za wananchi badala yake kuwashirikisha katika kurasimisha maeneo hayo.
No comments
Post a Comment