Writen by
sadataley
9:55 PM
-
0
Comments
IKULU, DAR ES SALAAM
Amirijeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dk John Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakub Hassan Mohammed kuwa Mnadhimu Mkuu mpya wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, pamoja na uteuzi huo amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na Luteni Jenerali na mteule huyo anachukua nafasi aliyokuwa nayo Luteni Jenerali Aloyce Mwakibolwa ambaye amestaafu.
Aidha, Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;
1.Brig Jen. J.G. Kingu, 2. Brig Jen. M.S. Busungu, 3. Brig Jen. R.R. Mrangira, 4. Brig Jen. B.K. Masanja, 5. Brig Jen. G.T. Msongole, 6. Brig Jen. A.F. Kapinga 7. Brig Jen. K.P. Njelekela, 8. Brig Jen. A.S. Bahati, 9. Brig Jen. M.E. Mkingule, 10. Brig Jen. S.S. Makona
Taarifa ya Ikulu imesema, Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ LuteniJenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments
Post a Comment