Writen by
sadataley
9:24 AM
-
0
Comments
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo ya Mpango wa Chakula, (WFP), Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) na Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinaadamu (OCHA) yamesema kwamba, nchi za kusini mwa Afrika zinakabiliwa na hatari ya kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Taarifa ya mashirika hayo imeeleza kwamba, ukosefu wa mvua mwishoni mwa mwaka 2017 na mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 unahatarisha uzalishaji wa chakula kwa nchi za kusini mwa Afrika.
Mpango wa Chakula, (WFP), umeeleza kwamba, uhaba huo wa mvua unatiashia uhai wa mamilioni ya raia wa kusini mwa Afrika wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Katika ripoti yao mashirika hayo kwa pamoja yamesema kuwa, mabadiliko ya tabianchi kama vile ukosefu wa mvua na ongezeko la joto kusini mwa bara la Afrika vimesababisha upungufu mkubwa wa uzalishaji wa mazao katika nchi za jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC.
Katika ripoti yao mashirika hayo kwa pamoja yamesema kuwa, mabadiliko ya tabianchi kama vile ukosefu wa mvua na ongezeko la joto kusini mwa bara la Afrika vimesababisha upungufu mkubwa wa uzalishaji wa mazao katika nchi za jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC.
Nchi zinazokabiliwa na hatari hiyo ya uhaba mkubwa wa chakula ni Botwana, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini na Zimbabwe.
WFP imesema kutokana na mabadiliko ya ghafla ya tabianchi baadhi ya wazalishaji wakubwa kama Afrika Kusini wameripoti kuporomoka kwa uzalishaji wa mahindi kwa asilimia 22, jambo ambalo litaathiri eneo kubwa la nchi za kusini mwa Afrika zinazotegemea nafaka ya mahindi kama chakula kikuu.
Kwa pamoja mashirika hayo yametoa wito kwa nchi za SADC na wadau wengine kutafuta njia mbadala ya kuweza kuokoa uzalishaji wa mazao na mifugo kusini mwa Afrika ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaotegemea kilimo katika ukanda huo.
Parstoday
No comments
Post a Comment