Saturday, February 17, 2018

Udart yamwaga mabasi 70 Dar

Kampuni itoayo huduma ya usafirishaji wa abiria kwa mabasi ya mwendo wa haraka jijini Dar,(Udart) imeingiza mabasi mapya 70 na kuyapokea bandarini jijini Dar katika kuhakikisha inaongeza nguvu na kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wateja wake.

 Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuyapokea mabasi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, Charles Selemani amewashukuru wakazi wa Dar kwa kuendelea kutumia usafiri huo na kwamba wazidi kuwa na imani juu yao ikiwa ni pamoja na kuwa wavumilivu kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na usafiri huo kwani siku si nyingi mikakati hiyo itakamilika.

 Aidha, Bw. Selemani ametoa ufafanuzi kuwa mabasi hayo yana uwezo wa kubeba abiria 150 hadi 160 ambapo yatasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa kuajiri idadi kubwa ya vijana wa Kitanzania na hivyo kuchangia uinuaji wa uchumi ndani na nje ya Jiji la Dar.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment