Writen by
sadataley
5:28 PM
-
0
Comments
Mubarak akana kuarisha mauaji Msiri.
Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak amekana kuwa hakuamrisha
maafisa wa Usalama wawashambulie waandamanaji mwaka wa 2011.
Mubarak mwenye umri wa miaka 86 alijitetea kuhusu vitendo vyake katika kesi
inayomkabili akisema kuwa hakuagiza mauaji ya mamia ya waandamanaji .Mubarak amesema kuwa alikubali kuwacha mamlaka mnamo mwaka 2011 ili kuzuia umwagikaji wa damu.
Bwana Mubarak alikuwa akizungumza katika kesi yake ambapo anashtakiwa kwa kupanga njama ya kuwaua mamia ya waandamanaji.
Mubaraka aliondoka malakani baada ya siku 18 ya maandamano huku watu zaidi ya 350 wakiwawameuawa katika makabiliano na vyombo vya usalama.
Mubarak akana kuarisha mauaji Msiri.
Rais huyo wa zamani alipatikana na hatia miaka mitatu iliyopita lakini uamuzi huo ukabatilishwa mwaka uliopita.
Kesi itaamuliwa tarehe 27 mwezi septemba.
Mubaraka alihutubia mahakama kwa takriban dakika 25 akiwa katika kiti chake cha magurudumu .
Aliiambia mahakama kuwa alikuwa ameitumikia serikali ya misri maisha yake yote lakini anastaajabu kwanini wakati wake wa mwishomwisho ndipo anapohangaishwa.
Kulingana naye anauhakika kuwa nafsi yake ni shwari.
No comments
Post a Comment