Writen by
sadataley
5:49 PM
-
0
Comments
Rais Jakaya Kikwete
Na Daniel Mjema, MwananchiDodoma. Masikio ya Watanzania leo yanaelekezwa mjini hapa
kusikia kile ambacho Rais Jakaya Kikwete alisema ni hatima ya mchakato
wa Katiba, atakapokutana na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
TCD inaundwa na vyama vya siasa vyenye wabunge kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Mazungumzo hayo yaliyopangwa kuanza saa 6.00
mchana Ikulu ndogo, ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa Bunge Maalumu la
Katiba lisitishwe kupisha uchaguzi mkuu kwa kutumia Katiba ya mwaka 1977
au la.
Habari kutoka ndani ya TCD zinaeleleza kuwa
mazungumzo hayo yanatarajiwa kutanguliwa na kikao cha juu cha taasisi
hiyo kilichopangwa kufanyika jana katika Hoteli ya St.Gasper kuanzia saa
10.00 jioni.
“Kikao cha leo (jana) cha Summit ya TCD ni kwa
ajili ya kupokea na kuidhinisha maazimio ya Kamati Ndogo ya watu wanne
iliyoundwa kupitia mambo yaliyojitokeza katika kikao cha kwanza na Rais
Kikwete,” alisema mtoa habari wetu.
Kamati hiyo inamjumuisha katibu mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, katibu mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa,
mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia. “Hiyo kamati iliundwa kufanyia kazi
mapendekezo ya Rais baada ya kukutana naye. Tunaamini kwa kusaidiana na
wataalamu wake, Rais alikwenda kuyafanyia kazi yale tuliyoyapendekeza
kama TCD,” alisema mmoja wa viongozi.
Akihutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dodoma
wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema leo ndiyo itakuwa hatima ya
mazungumzo hayo.
Chanzo kingine cha habari ndani ya TCD
inayojumuisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) uliosusia vikao vya
Bunge hilo, kimedokeza kuwa suala la kufanya uamuzi mgumu kuhusu
mustakabali wa Bunge kwa masilahi ya Taifa, lipo mikononi mwa vyama vya
siasa badala ya wajumbe.
“Ukiwauliza wajumbe kama Bunge liahirishwe au la,
watataka lisiahirishwe kwa sababu wanafikia ukomo na baadhi hawana
uhakika wa kurudi,” alisema mpashaji huyo.
No comments
Post a Comment