Sunday, July 19, 2015

KUNDI LA 4UMOVEMENT DAR LATANGAZA KUUUNGA MKONO UKAWA

TAARIFA RASMI - 4U MOVEMENT TANZANIA 4u movement Tanzania inajipambanua katika mabadiliko chanya kwa nchi yetu, tumeongoza Kuyasaka mabadiliko Kupitia balozi wetu wa mabadiliko Mh Edward Lowassa ndani ya CCM. Mchakato wa Kidemokrasia wa kudai mabadiliko ndani ya CCM umefungwa bila balozi wetu kuwa mpeperusha bendera hio na si kwa kushindwa , bali haki haikutendeka kwake na kwa wagombea wengine kwa kufinyangwa kanuni za chama katika Mchakato. Tuliahidi kuto rudi nyuma na kamwe hatuwezi saliti nchi yetu, Mwl Julius Kambarage Nyerere muasisi wa Chama Cha Mapinduzi na Baba wa Taifa alituasa, tukiyakosa mabadiliko ndani ya CCM tuwe radhi kuyatafuta nje ya CCM. 4u movement Kama vuguvugu la mabadiliko hatusimami kuyadai mabadiliko ndani ya nchi yetu. Tunaanza rasmi safari ya kudai mabadiliko nje CCM kwani si dhambi na ni haki yetu ya kikatiba. Tunawaomba wana 4umvt kwenda kushiriki kikamilifu uchaguzi wa 2015 kwa kuchukua fomu mbali mbali za uchaguzi, Kujiandikisha kWa wingi na kuwa hamasisha wenzetu wajiandikishe ili kwenda kutafuta mabadiliko YA kweli na kuingoa CCM madarakani. Chanzo:chadema blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment