Writen by
sadataley
5:23 PM
-
0
Comments
WANAHABARI mkoani Iringa wamemchangia zaidi ya Sh 600,000 mwanahabari Frank Kibiki, aliyechukua fomu kugomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili agombee ubunge wa jimbo la Iringa mjini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoani Iringa, Frank Leonard alisema mchango wao ni kwa ajili ya kumsaidia mwenzao, ili aendee kupambana na kinyang’anyiro hicho.
“Tupo tayari kukusapoti mwenzetu na tunakupa hongera sana kujitosa kwenye kinyang’anyiro hiki hasa katika jimbo linaloonekana gumu kama Iringa mjini,”alisema
Leonard aliwapongeza wanahabari wote waliojitosa kugombea majimbo malimbali nchini.
Kwa upande wake Kibiki, aliwashukuru wanahabari kwa mchango wao mkubwa, na kwamba tangu kutangaza nia amekuwa akipata ushirikiano ambao, anaamini utaendelea mpaka mwisho na sio kwake tu hata kwa wanahabari wengine.
“Nawashukuru wanahabari kwa mchango wao mkubwa kwangu, nikitaja majina ya vyombo sitamaliza lakini redio, magazeti, tv, blogs na vyombo vingine wamenisaidia sana, huu ni ushirikiano ambao hatupaswi kuuacha hasa mwenzetu mmoja anapoamua kufanya ,” anasema
Alisema ameamua kugombea ubunge ili apate nafasi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Iringa mjini, ambao wanahitaji mbunge aliye mtumishi wao.
Kibiki alisema anajivunia uzoefu wa uongozi ambao ameupata kupitia nafasi yake ya Ukatibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wa wilaya alioutumikia kwa zaidi ya miaka 10 na nafasi ya afisa mtendaji wa kata, aliyofanya kwa mwaka mmoja.
Alisema kipaumbele chake ni kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo, katika kupambana na changamoto nyingi zinazowagusa vijana, wanawake, walemavu, wazee na makundi mengine kwenye jamii ya jimbo lake ikiwa atapata ridhaa ya kupitishwa na chama chake hatimaye kushinda uchaguzi mkuu wa October.
Mwisho.
Chanzo:mwitikio blog
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment