Writen by
sadataley
4:02 PM
-
0
Comments
MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka Walimu wa Shule ya
sekondari Ismani wilaya ya Iringa kukutana kuweka mikakati itakayo
iwezesha Shule hiyo kuingia katika Shule 10 bora Kitaifa.
Huku akipiga marufuku maandamano ya Walimu ndani ya Mkoa wa Iringa kwa kisingizio cha kudai haki pasipo wajibu.
Akizungumza Leo na Walimu wa Shule ya sekondari Ismani Mkuu huyo wa Mkoa alisema amepata kusikia katika Vyombo vya Habari kuwa kuna Walimu wanahamasishwa kufanya maandamano ya kudai Haki zao.
Alisema kuwa kimsingi hakuna Kiongozi anayewazuia na asiyependa Walimu waliotimiza wajibu wao na kufuata taratibu za kudai madai yao kunyimwa haki yao.
Hivyo haoni sababu ya wao kuandamana barabarani badala ya kutumia njia sahihi ya kuikumbusha serikali kuwalipa madai yao bila wao kuandamana.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema baadhi ya Walimu madai yao wanayodai hayapo kwenye mafaili yao na hayatambuliki hivyo kwa wakati mwingine mwalimu anapokwenda kutibiwa nje ya kituo chake cha kazi ni lazima aende kwa utaratibu na kumbukumbu za madai yake kuweka kwenye faili lake.
Pia alisema lazima kuweka mkakati wa Walimu kujiwekea mikakati ya kuifanya Shule hiyo kuwa nafasi ya 10 bora na njia pekee ambayo amewaagiza wakurugenzi ni kuingia mikataba na Walimu hao na yeye kuingia mkataba na wakuu wa wilaya.
Kwa Walimu alitaka kuendelea kuongeza jitihada za kufundisha ili hata wale wenye Sifa ya kupandishwa daraja wapandishwe kutokana na uwezo wao kikazi na si vinginevyo.
Alisema kuwa suala la Walimu kupandishwa madaraja limesitishwa kwa ajili ya kupisha uhakiki wa watumishi hewa na baada ya kukamilisha zoezi hilo watafahamishwa wote wenye Sifa ya kupandishwa daraja.
Aidha alionya Walimu kuendelea kupoteza muda wao kwa kushinikizwa kufanya maandamano.
"Najua kuna mtu yupo nyuma yenu anawachochea kufanya mgomo huu ila yeye si mwalimu na hana madai yoyote anayoidai serikali"
Kuhusu upungufu wa Walimu wa somo la Sanyansi na Hesabu kwa Shule hiyo yenye Walimu wanne pekee alishauri uongozi wa Shule hiyo kuendelea kuwatumia Walimu wa Chuo cha Mkwawa ambao wapo masomoni kwa ajili ya kupunguza upungufu wa Walimu shuleni hapo.
Awali akizungumza na wanafunzi wa Shule hiyo mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa juhudi na kuachana na mafataki wakiwa Shule.
Kwa upande wake mwalimu Erick Mlelwa alimwomba mkuu huyo wa mkoa kumsaidia kufuatilia sababu za kusitishiwa mshahara wake kwa zaidi ya miezi nane sasa.
Akimjibu mwalimu huyo baada ya taarifa toka kwa Afisa elimu sekondari wilaya kuwa alisitishiwa mshahara kutokana na utoro alisema kuwa alichokitafuta mwalimu huyo amekipata kutokana na utoro wake ambao hata yeye hakubali kuona mtumishi mtoro katika Mkoa wake.

No comments
Post a Comment