Writen by
sadataley
12:30 PM
-
0
Comments
Wamarekani waliowengi wanaamini kuwa kiwango cha chuki kimeongezeka nchini humo baada ya kuchaguliwa Donald Trump kama rais.
Asilimia
63 ya wapiga kura Marekani wanasema kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la
chuki na taasubi tokea Trump achaguliwe Novemba 2016 huku asilimia 32
wakiamini kuwa hakuna chochote kilichobadilika.
Kwa
mujibu wa uchunguzi huo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac huko
Connecticut, asilimia 77 ya Wamarekani wanaamini kuwa watu wa jamii za
waliowachache wanaonewa na kudhulumiwa.
Wataalamu wanasisitiza kuwa, matamshi ya kibaguzi ya Trump pamoja na sera zake ni chanzo cha chuki, mashambulizi na hujuma zinazofanywa na makundi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani.
Chanzo: parstoday.com
No comments
Post a Comment