Writen by
sadataley
12:32 PM
-
0
Comments
Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewakamata Wapalestina kadhaa akiwemo mbunge mwanamke.
Mjumbe
wa Bunge la Palestina Bi. Samira al Halayka ambaye ni mwanachama wa
Hamas, alikamatwa Alhamisi akiwa nyumbani kwake katika mji wa
al-Shoyoukh katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Duru zinadokeza kuwa mbunge huyo alifungwa pingu kisha akafunikwa macho na kupelekwa kusikojulikana na wanajeshi hao wa Israel.
Taarifa zinasema wanajeshi wa Israel pia walipora kompyuta yake na simu yake ya mkononi katika oparesheni hiyo ya utekaji nyara.
Kwa ujumla kuna Wapalestina karibu 7,000 katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Chanzo: parstoday.com
No comments
Post a Comment