Writen by
sadataley
1:29 PM
-
0
Comments
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesisitiza haja ya kuimarisha mashirikiano kwa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA), hatua ambayo
itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi kwa nchi hizo sambamba na
kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo.
Dk.
Shein aliyasema hayo leo katika Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi na
Serikali wa Jumuiya ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),
unaofanyika Mjini Jakarta Indonesia, mkutano ambao unaenda sambamba na
maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo.
Pia
Dk. Shein alisema kuwa umefika wakati kwa nchi hizo wanachama wa
Jumuiya ya IORA kuimarisha zaidi ushirikiano pamoja na kutatua
changamoto zilizopo zikiwemo hali ya usalama, kupambana na uharamia
baharini , vita dhidi ya madawa ya kulevya, Ugaidi, athari za tabia nchi
na mambo mengine yanayoweza kuleta athari katika nchi wanachama.
Dk.
Shein, alitoa wito kwa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya IORA kuongeza
kasi katika utekelezaji wa malengo na maazimio ya Jumuiya hiyo ikiwa ni
pamoja na kuitekeleza dhana ya uchumi wa habari iliyoanzishwa mwaka 2015
na Jumuiya hiyo.
Kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Dk. Shein alisaini makubaliano yaliyofikiwa na Jumuiya hiyo
katika Mkutano huo na kuahidi kwa Tanzania itachukua juhudi za makusudi
katika kuyatekeleza makubaliano hayo kwa lengo la kuimarisha Jumuiya
hiyo.
Chanzo:CCM Blog
No comments
Post a Comment