Writen by
sadataley
1:27 PM
-
0
Comments


The beginning of every government starts with the education of our youth.
(Mwanzo wa kila serikali unaanza na kuwapatia elimu vijana wetu)
—Pythagoras
(Mwanzo wa kila serikali unaanza na kuwapatia elimu vijana wetu)
—Pythagoras
Katika kitabu chake cha “Think Like a
Champion” yaani fikiria kama mshindi, mwandishi Donald J. Trump ambae
kwa sasa ni Rais na Amri Jeshi mkuu wa taifa tajiri na nguvu za kijeshi
la Marekani, amenukuu falsafa ya Pythagoras.
Muandishi Donald Trump, amehimiza
umuhimu kwa kujifunza na kuoanisha aina ya kujifunza kama mwanzo mpya
kwenye kila zama ambayo mtu unaingia. Katika kitabu hicho Donald Trump
ameonesha jinsi Pythagoras aliekuwa nguli wa falsafa hususani katika
somo la hisabati, mara nyingi alitafsiri mambo mengi kwa kuoanisha au
kuwakilisha na tarakimu au nambari.
Donald Trump yeye kama mfanya biashara
nyakati ameandika na kupiga chapa kitabu kicho yaani mwaka 2009
ameonesha kuwa kuna muunganiko wa moja kwa moja kati ya elimu inayompa
mtu mmoja mmoja maarifa hali kadhalika jamii nzima kupata maarifa
kupitia mifumo mbalimbali ya elimu.
Mie ninaendika makala hii kwa uzoefu na
ujuzi niliopata wakati nasoma chuo cha ualimu na baadae kupata mafunzo
ya taaluma nyingine, naweza kurejea jambo ambao nimewahi kuandika huko
nyuma kuwa sisi wanadamu, tuna namna ya kujifunza shule au vyuoni
(formal education), kuna namna ya tunajifunza kwa malengo maalum ili
kupata ujuzi tunaoutaka (non-formal education). Vilevile tunaweza
kujifunza kwa kupitia vitabu, majarida, mitandao ya kijamii, program za
radio, televiseni n.k na hii inaitwa (informal education). Vyovyote
vile, maarifa tunayoyapata yanatakiwa kutubadilisha namna ya kufikiri na
kuzalisha mabadiliko ya kitabia.
Trump, alijikita katika kusisitiza kila
mtu anapoanza jambo jipya, kuna umuhimu wa kujifunza au kujiongezea
maarifa mapya kuhusiana na mambo mapya anayotaka kuyafanya. Mwandishi
ambae ni Rais wa awamu ya 45 kwa sasa ya Marekani amejielezea kwa uzuri
namna ambavyo amekuwa katika kujifunza ujenzi wa nyumba na hoteli ili
anapokuwa na wahandisi-wajenzi walau asiachwe nyuma na lugha za kimsingi
za kiufundi hasa katika ujenzi.
Kuna nyakati alijikita katika
uendelezaji wa viwanja vya gofu, ilimlamlazimu pia atafute kundi la
wataalamu wa kucheza mchezo wa gofu na wajenzi wa viwanja wa gofu. Lengo
lake, ilikuwa ni kukaa na wataalamu kwa lengo la kupata taarifa za
msingi kutoka kwenye uzoefu wa sekta au biashara ambayo alikusudia
kuifanya.
Donald Trump aliamini na anaamini sana
katika hisia mpya huwa zinajengwa katika misingi ya mwanzo mpya na
mwanzo mpya umeunganishwa na maarifa mapya yanayopelekea namna mpya ya
kufikiri na namna mpya ya kutenda ili kupata matokeo mapya.
Haina tofauti na msemo wa kibiblia wa
umuhimu wa divai mpya katika chupa mpya ili kupata matokeo tarajiwa.
Tofauti na divai mpya unaweka katika chupa ya zamani. Inapelekea
kupoteza divai na chupa hali kadhalika.
Natamani kununua au kuazima uzoefu wa
falsafa ya Donald Trump katika muktadha wa Tanzania ya Rais John Pombe
Magufuli na Watanzania walio wengi.
Kuna namna Mheshimiwa Rais ameingia
darasani kama mwalimu na anatoa mafunzo kwa chaki ubaoni. Wakati Mwl.
Magufuli anafundisha kwa mujibu wa mungozo mpya wa somo (new syllabus)
kwa upande mwingine wanafunzi ambao ni Watanzania wanakumbuka mafunzo na
malezi ya Mwl. Jakaya Mrisho Kikwete ya awamu ya 4. Na wengi wakitaka
kuishi kama awamu ya 4.
Falsafa ya Mwl. Kikwete ilikuwa 1+ ( ) =
5. Wanafunzi ambao ni Watanzania tulikuwa na jukumu la kufikiri ni
namba ngapi ikijumlishwa na moja tunapata 5. Kwa muongozo wa kujifunza
haukuhitaji njia ya kuonesha jibu ambalo ni 4 umelipataje. Na kwa
muongozo wa mafunzo yale, ukiweka 4 mwalimu atakupa vema kwa kuwa jibu
ililoweka ni sahihi.
Mara hii ameingia Mwl. Magufuli ambae
ana swali kama lile la mwalimu wa awamu ya nne, isipokuwa badala ya
parandesi, wakati swali lina herufi X
1+X = 5.
1+X = 5.
Mwalimu Magufuli anataka utafute thamani ya X kwa njia za kihisabati za jiometri.
Sote tunakubaliana kuwa thamani ya X ni 4, isipokuwa njia ya kuifikia 4 ni tofauti na muongozo wa mafunzo ya Mwl. Kikwete.
Awamu ya 5 anatutaka ili kupata jibu,
sisi Watanzania ambao ni wanafunzi darasani, tuna wajibu wa kujua kwamba
tunatakiwa kuonesha njia ya kulifikia jibu ambalo ni 4.
Kwa lugha rahisi inatakiwa kuchukua swali 1+X = 5 na kutoa 1 kila upande
1+ (-1)+ X = 5 – 1
Jibu litakalopatikana litakuwa wazi kabisa kuwa
0 + X = 4
Hivyo basi kumbe thamani ya X = 4.
Huu ndiyo mfumo wa muongozo wa mafunzo
anayotumia mwalimu wa awamu ya 5. Kuna uwezekano kutokana na wepesi wa
masomo awamu ya 4, kuna nyakati mwalimu alihitaji tuimbe nyimbo kama
sehemu ya kujifunza.
Isipokuwa muongozo wa kujifunza na
kufundishia uliopo sasa watutaka tujue namna tofauti ya kutafuta thamani
ya X. Muongozo wa mwalimu hautupi fursa ya kuimba kama namna ya
kujifunza kama kule nyuma. Na hapa ndipo tofauti inapoanza kuonekana
kwani baadhi ya wanafunzi bado wanatamani uji kumbe tupo katika zama za
kula ugali na nyama ya mifupa. Tunawajibika kutumia meno yetu kutafuna
kuitoa nyama katika mifupa.
Wanafunzi darasani (yaani Watanzania
wengi) bado wanataka mwl. Magufuli afundishe kama mwl. Kikwete na
kutumia njia za zamani kuja na jibu la thamani ya X.
Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu ambao
ni wanafunzi katika darasa la mwalimu wa awamu ya 5; chonde chonde, tuna
jukumu moja kubwa la kufanywa upya namna ya kufikiri. Namna pekee ya
kufikiri na kukubaliana na ukweli, mfumo mpya wa muongozo wa mafunzo
ndivyo unavyotaka, na mwalimu tulie nae, muongozo wa masomo na mbinu
zake za kujifunzia si kuimba (nibebe nibembeleze kama wimbo mmoja
uliowahi kutamba katika nyimbo za injili).
Tukiji-position kwa kujua tupo awamu ya 5
na kuamua kujikita katika mbinu mpya za kukokotoa ili kupata majibu;
tukifanya hivyo bila shaka lawama na manung’uniko yataisha. Na
tutajikuta tunawajibika na kujituma kwa kutumia mbinu halali na njia
halali ya kufikia jibu.
Tukigoma kujifunza, tunajiweka katika hali ya kutokua kiufahamu hususani kwenye kukabiliana na changamoto zinazotuzunguka.
Tunaweza kupata jibu la changamoto
nyingi ikiwemo kutengeneza hela kihalali bila kutumia njia za mkato pale
tu tunapojua, awamu hii na muhula huu, unahitaji mtanzamo mpya katika
utatuzi wa matatizo yanayotuzunguka.
Na utatuzi unapofanyika, maana yake njia ya kufikia jibu inatakiwa kuwa wazi ili mtu yeyote anaekagua namna mwanafunzi alivyopata jibu, bila maswali ya ziada aone jibu lilivyopatikana.
Na utatuzi unapofanyika, maana yake njia ya kufikia jibu inatakiwa kuwa wazi ili mtu yeyote anaekagua namna mwanafunzi alivyopata jibu, bila maswali ya ziada aone jibu lilivyopatikana.
Ili tufaulu hisabati za mwl. Magufuli
hatuna budi kumpenda na kumkubali kuwa ndiye mwalimu wetu na
tunawajibika kukubaliana na mbinu zake za kufundishia na kujifunza ili
kupata matokeo tunayotarajia.
Wataalamu wa saikolojia wanaonesha kuwa,
wanafunzi hufaulu vyema pale wanapokuwa na uhusinaano mzuri na mwalimu
huhusani kwa kumpenda na kushirikiana nae hata nje ya saa za darasa kwa
kwa nia njema ya kujifunza ili kutatua mafumbo kwa lengo la kupata
majibu.
Chuki kwa mwalimu hupelekea kuchukia
somo vilevile, na hatimaye kushindwa kukabili changamoto za masomo.
Ufaulu wa masomo ni faida ya mwanafunzi kupata daraja zuri au alama
nzuri. Ufaulu wa kutatua changamoto zinazotuzunguka, sisi wanafunzi
(Watanzania) ni wafaidika wa kwanza.
Hii yanikumbusha siku chache zilizopita
nilipata kuhudhuria mafunzo yaliyokuwa yakifanywa na maafisa wa kijeshi.
Moja ya kitu nilichopata katika mafunzo yale, ni namna wapiganaji hao
wanavyofikiri ili kupata majibu ya utatuzi wa maswali magumu au
changamoto mbele yao.
Afisa mmoja akatoa mfano, ukikutana na
mto wenye mamba wakali na unatakiwa kuvuka upande wa pili wa mto; Je
utapita katikati ya maji ili mamba wakutafune au utafanya nini. Afisa
yule wa kijeshi akaweka wazi kuwa, kuna namna ya kuishughulisha akili
ili kupata suluhisho la kusonga mbele na kuendelea na safari ili kufika
kule unakotaraji.
Moja ya suluhisho lililotolewa na mpiganaji yule ni kurusha kamba upande wa pili wa mto na kuifunga kamba nyingine kwenye kipago au mti mubwa na kisha kuvuka kwa kutambaa kwa miguu na mikono kwenye kamba huku mamba wakikukodolea macho unapopita juu yao.
Moja ya suluhisho lililotolewa na mpiganaji yule ni kurusha kamba upande wa pili wa mto na kuifunga kamba nyingine kwenye kipago au mti mubwa na kisha kuvuka kwa kutambaa kwa miguu na mikono kwenye kamba huku mamba wakikukodolea macho unapopita juu yao.
Kwa mtu mwingine angeweza kurudi
alikotoka, mwingine angeweza kutupa lawama ooh… kuna mamba kwenye mto,
na mie siwezi kuvuka. Tofauti ya kufikiri kwenye tatizo lile lile ndilo
linawafanya Wanajeshi kujiona washindi na akili zao zimejiengwa kusonga
mbele hata pale mambo yanapokuwa magumu. Hivyo kurusha kamba upande wa
pili na kisha, anavuka kwa kamba ni moja ya mbadala katika mbinu mpya ya
kutatua tatizo la mto wenye mamba.
Katika nyakati hizi, tuna wajibu wa
kufikiri kwa kiwango sawia na muongozo wa somo la awamu ya 5. Moja ya
assignment (homework) aliyoitoa mwalimu Magufuli wakati mmoja akiongea
na wahariri, ni waandishi kufungua kampuni ili kujenga viwanda au kuwa
na shughuli ya uzalishaji mkubwa unaotoa ajira kwa vijana na kuongeza
thamani ya malighafi hasa za mazao ya kilimo na mifugo. Nae Mheshimiwa
Rais alitoa ahadi ya kusaidia mchakato ili kampuni hilo lipate mkopo
kutoka benki ya ukekezaji. Je kuna, mtu au waandishi wameshapeleka
andiko la mradi wa kampuni na mwalimu wetu wa darasa la awamu ya 5
akashidwa kutoa msaada? Au ndiyo wengi wanatumia kalamu na keyboard za
social media kulalamika tu?
Kumbe tunaweza pia kungusha mti na
kuulaza upande mmoja wa mto kwenda upande mwingine na kuvuka kwa
kutambaa juu ya gogo la mti na kuendelea na safari ya maisha pasi
kulalamika kwanini mwalimu anatuelekezea njia ngumu za kupata matokeo.
Mungu ibariki Tanzania. Tuna jukumu la
kumkubali mwalimu wetu ili tufaulu mitihani katika zama za mafunzo mapya
ili kupata alama nzuri na kusonga mbele katika hatua ijayo.
Fred Matujafmatuja@hotmail.com
Chanzo:Mjengwa Blog
No comments
Post a Comment