Writen by
sadataley
12:48 PM
-
0
Comments
Kinara wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ameukimbia mji wa Mosul, Iraq kwa msaada wa askari wa Marekani katika eneo hilo.
Hayo yamedokezwa na Jawad Al Talibawi kamanda wa Wapiganaji wa vikosi vya kujitolea
vya wananchi Iraq maarufu kama Al-Hashd Al-Shaabi ambaye ameongeza
kuwa, wanajeshi wa Marekani wamemsaidia Abubakar Al Baghdadi kutoroka na
kujificha katika eneo la Al-Qayrawan. Amesema taarifa za
kijasusi zinaonyesha kuwa kinara huyo wa ISIS yuko baina ya Al-Qayrawan
na eneo la Al Hadhr yapata kilomita 80 kusini mwa Mosul.
Siku ya
Jumatano, Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon ilisema kuna uwezekano
kuwa Al Baghdadi ameondoka Mosul na kujificha katika maeneo ya jangwani
nje ya mji huo. Siku chache zilizopita Al Baghdadi alitoa hotuba ya
mwisho akikiri kushindwa kundi hilo nchini Iraq na akiwataka wafuasi
wake kukimbilia maeneo ya milimani kwa usalama wao au kujiripua.
Chanzo:parstoday.com
No comments
Post a Comment