Writen by
sadataley
7:31 AM
-
0
Comments
Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania.
Katika muswada huo, Bhanji
ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka
Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu.
Muswada huo kama utapitishwa na
Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika
kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye
Ualbino.
“Ninamshukuru Mungu kwa fursa hii,
” anasema Bhanji huku akisema kwamba kwake yeye jana ilikuwa ni siku ya
furaha kubwa kwani hatimaye aliweza kuwasilisha bungeni muswada huo
binafsi ambao unaoitwa The EAC Protection Of People with Albinism Bill
2017.
Mwanamuziki mahiri nchini Chege
Chigunda aliandika katika page yake ya Instagram ambapo alimpongeza
mbunge huyo kwa namna anavyofikiri na kutetea walemavu aliandika:
“Hongera sana Mbunge wetu wa
Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji @shyrosebhanji kwa kupigania haki
za ndugu zetu wenye ualbino. Hakika umeacha alama kubwa ya uwakilishi
wako Tanzania na Afrika Mashariki. Tunajivunia.”
Habari kwa hisani ya Fullshangwe Blog
No comments
Post a Comment