Writen by
sadataley
7:33 AM
-
0
Comments
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama
akizungumza katika mkutano mkuu wa9 wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya
watumishi wa serikali za mita,LAPF jijini Arusha
Mkurugenzi wa KeyMedia Agency ya
jijini Arusha akiwa katikati Bi.Barbra Keiya wakiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa LAPF, kampuni hiyo ilibeba jukumu la kualika
vyombo vya habari kwaajili ya mkutano huo
Wakurugenzi wa KeyMedia Agency ya jijini Arusha Bi.Anna na Barbra wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja wa LAPF.
Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Bi.Jennista Mhagama amewataka vijana kujiepusha na madawa ya
kulevya ili utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda ilete ajira kwa
vijana wenye nguvu
Aliyasema hayo jijini Arusha wakati akifunga mkutano mkuu wa9 wa wadau
wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mita,
LAPF uliohudhuriwa na wadau wa mfuko huo
wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mita,
LAPF uliohudhuriwa na wadau wa mfuko huo
Alisema
kuwa kwa sasa serikali imedhamiria kuwainua idadi kubwa ya vijana
waliona ujuzu mdogo kwa kuwajenge uwezo kupitia mafunzo mbalimbali
katika vyuo vilivyopo nchini
”Udhibiti mkubwa wa madawa ya kulevya unahitajika kwa vijana wetu ili kutengeneza taifa lenye nguvu ya kufanya kazi ”alisema
Aliongeza
kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana ujuzi wa kutosha hivyo basi
serikali ya awamu ya 5 imejipanga ipasavyo kuhakikisha vijana wanapata
ajira kupitia viwanda
Hata
hivyo aliipongeza mfuko wa LAPF kwa kazi nzuri wanayofanya huku
akiitaka mifuko yote ya kijamii hapa nchini ihakikishe kuwa ifikapo 2025
inakuwa na wanachama wengi zaidi.
Chanzo: Fullshangwe Blog
No comments
Post a Comment