Writen by
sadataley
3:23 PM
-
0
Comments
Mchezaji
wa timu ya Mwadui FC, Hassan Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Februari kwa msimu wa 2016/2017.
Kabunda aliwashinda wachezaji Laudit Mavugo wa Simba SC na Ibrahim Ajib pia wa Simba SC.
Katika
mechi tatu ambazo Mwadui ilicheza kwa mwezi huo, Kabunda alicheza kwa
dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya pointi sita
zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika Msimamo wa Ligi kwa mwezi
huo wa Februari (kutoka nafasi ya nane hadi ya sita).
Kabunda
alifunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo tatu kati ya sita
iliyofunga timu yake. Kiungo huyo mshambuliaji alionesha nidhamu ya hali
ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi.
Kwa
kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000
(milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Tanzania.
Chanzo:Fullshangwe Blog
No comments
Post a Comment