Writen by
sadataley
3:14 PM
-
0
Comments
Watu saba wamekamatwa na Polisi nchini Uingereza kwa tuhma za kuhusika na shambulizi la kigaidi nje ya bunge la nchi hiyo jijini London siku ya Jumatano.
Polisi wanasema washukiwa hao
wamekamatwa jijini London na mjini Birmingham, huku idadi ya watu
waliopoteza maisha ikiwa wanne wala sio watano kama ilivyotangazwa hapo
awali.
Miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni
afisa wa polisi aliyedungwa kisu, lakini pia raia wengine wa kawaida
waliojipata katika eneo la tukio hilo katika eneo la Westminister na
kugongwa na gari.
Zaidi ya watu 20 waliojeruhiwa baada ya
kugongwa na gari na wengine kukanyagana, wameendelea kupata matibabu
katika hospitali mbalimbali jijini London.
Kuhusu aliyetekeleza uvamizi huo ambao Uingereza imesema ni wa kigaidi, aliuawa pia baada ya kupigwa risasi na afisa wa polisi.
Waziri wa Uingereza Bi.Theresa May amelaani shambulizi hilo matamshi ambayo pia yametolewa na viongozi wengine wa dunia.
No comments
Post a Comment