Writen by
sadataley
1:20 PM
-
0
Comments
.Waziri
wa Utalii wa Lebanon Avadis Kadanian ajipata mashakani baada ya kusema
kuwa amefurahishwa na matatizo yanayokumba Uturuki kipindi hiki .
Waziri huyo ametakiwa kujiuzulu kufuatia kauli zake zilizotajwa kuwa za kibaguzi.
Siku
ya Ijumaa waziri Kadanian alikuwa akizungumza katika kipindi cha
mahojiano na televisheni ya MTV Lebanon ambapo alikiri kuwa yeye binafsi
haipendi Uturuki na kwamba hawezi kuwakaribisha waturuki nchini
Lebanon.
"Siwezi
kuunga mkono kitu chochote kilicho na uhusiano na Uturuki ,iwe ni
bidhaa zao au hata watu wao sina uwezo wa kuwazuia raia wa Uturuki
kutokuja Lebanon lakini pia sina nia yakuwakaribisha katika uwanja wa
ndege ."
Kadanian
pia alisema kuwa atachagua Armenia alipoulizwa ikiwa akiwa katika hali
ya kuwa afanye uchaguzi baina ya Armenia na Lebanon .
Kauli
za chuki za waziri huyo zilizua hisia kali mitandaoni na kampeni ya
kumtaka kujiuzulu ilianzishwa Twitter kwa alama ya reli
'#Kadanianapologiseorresign'.
Ujumbe
mmoja wa Twitter pia ulifahamisha kuwa 'Haiwezekani waziri wa Lebanon
kuwa na kauli ya chuki kuhusu raia wa Uturuki wakati Lebanon na Uturuki
zina uhusiano mzuri.'
Waziri wa zamani wa sheria Ashraf Rifi alimtaka Kadanian pia kujiuzulu.

No comments
Post a Comment