Writen by
sadataley
8:12 AM
-
0
Comments
Duru za habari zimeripoti jinai mpya za kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) kwamba wanachama wa kundi hilo wanafanya majaribio ya silaha zao za kemikali kwenye miili ya wanadamu.
Nyaraka za siri ambazo zimefichuliwa hivi karibuni zinaonyesha kwamba kabla ya kundi hilo kutekeleza shambulizi la silaha za kemikali, huwa linazifanyia majaribio silaha hizo kwenye miili ya watu. Baadhi ya nyaraka hizo za maandishi zimenaswa na askari wa Iraq katika Chuo Kikuu cha Mosul, ambapo zilikuwa zimefichwa ikiwa ni baada ya kukomboa mji huo wa Mosul kutoka kwa wanachama wa kundi hilo la kigaidi.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wanachama wa Daesh huwalazimisha watu waliowashikilia kula mada ya 'Sulfate Thaliamu' ambapo baada ya kula mwili hupatwa na joto kali, kutapika, kusinyaa ubongo na utumbo na hatimaye kupoteza maisha siku chache baadaye kwa namna ya kutisha sana. Aidha wanachama wa kundi hilo huwachoma watu sindano ya sumu iliyochanganywa na mada ya 'Nikotini' na kupoteza maisha ndani ya saa chache tangu kufanyiwa ukatili huo. Baadhi ya weledi wa mambo wameelezea vitendo vya kujaribu silaha za kemikali vinavyofanywa na wanachama wa genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS), kuwa vinavyokumbushia vitendo kama hivyo vya Wanazi wa Ujerumani enzi za utawala wa Hitler.
Inafaa kuashiria kuwa, silaha za kemikali zimekuwa zikitumiwa na magaidi kwa ajili ya kuzihadaa fikra za walio wengi duniani, ambapo baada ya kutekeleza jinai hizo, magaidi na washirika wao yaani Marekani na mataifa mengine, huituhumu serikali ya nchi ilikotendwa jinai hiyo kuwa ndio iliyohusika.
No comments
Post a Comment