Tuesday, June 13, 2017

Familia zatengana kutokana na mzozo wa Qatar

Familia kadhaa nchini Qatar na mataifa mengine ya ghuba ya Kiarabu zalazimika kutengena kufuatia vikwazo vilivyowekwa tangu mzozo huo kuanza mapema juma lililopita .

Nchi zote zilizowekea Doha vikwazo vimetoa wito kwa raia wake kurudi katika nchi zao la sivyo uraia wao katika nchi za kwao utatupiliwa mbali.

Qatar,Kuwait,Saudi Arabia,Milki za kiarabu na Bahrain ni nchi ambazo zimeunganishwa kwa nyanja mbali mbali kama ufalme,makabila,ukoo na ndoa .

Kufuatia mzozo wa Qatar familia nyingi zimelazimishwa kutengana baada ya vikwazo kuwekwa na kusitisha uhusiano wa aina yoyote .
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment