Ikulu ya White House Marekani yakanusha kuairishwa kwa ziara ya rais Donald Trump nchini Uingereza
Rais wa Marekani Donald Trump hakuzungumzia kuhusu uwezekano wa kuairishwa kwa ziara yake nchini Uingereza.
Taarifa zilizotolewa na ikulu zilifahamisha kuwa rais Donald Trump na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May hawakuzungumzia kuhusu suala hilo.
Ikulu ya White House imekanusha taarifa zilizozagaa kuwa Donald Trump anahofia maandamano dhidi yake nchini Uingereza na kuairisha ziara yake.
Malkia wa Uingereza Elizabeth II alimualika Donald Trump wiki moja baada ya kuapishwa kuwa rais wa Marekani.
Licha ya mualiko huo hadi kufikia sasa hakuna tarehe iliopangwa kufanyika ziara hiyo.
No comments
Post a Comment