Tuesday, June 13, 2017

UN yasema UAE imekiuka vikwazo vya silaha Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema Umoja wa Falme za Kiarabu umekiuka vikwazo vya silaha dhidi ya Libya kwa kupeleka helikopta, ndege ya kivita na magari ya deraya nchini humo.
Ripoti ya baraza hilo imesema UAE imekuwa ikituma silaha hizo kwa jeshi la wanamgambo linalojulikana kama Jeshi la Kitaifa Libya (LNA) ambalo linasimamiwa na Jenerali Khalifa Haftar mashariki mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Ripoti hiyo yenye kurasa 300 ina ushahidi kuhusu namna pande hasimu katika mgogoro wa Libya zimekuwa zikipokea silaha kinyume cha azimio la Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo ilitazamiwa kutangazwa katika siku za usoni.
Baraza la Usalama liliiwekea Libya vikwazo vya kununua silaha kufuatia vita vya ndani vilivyoibuka nchini humo mwaka 2011.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inasema UAE ilimpa Jenerali Haftar helikopta kadhaa ikiwemo ya mzinga ya Mig-24 iliyoundwa Russia pamoja na ndege moja ya kivita. Aidha UAE ilimpa Haftar magari 90 ya deraya na mengine 500 ya kijeshi. Kupewa nguvu wanamgambo wanaosimamiwa na Haftar ni jambo ambalo linadhoofisha jitihada za Algeria na Tunisia za kuutafutia suluhisho la kisiasa mgogoro wa Libya.
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment