Thursday, July 6, 2017

Wauwaji Kibiti watapatikana tu- Kassimu Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelaani na kusikitishwa na mauaji yanayotokea katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani na kusema kuwa wanaofanya mauaji hayo hata wakimbie watapatikana na kuchukuliwa hatua.

Hayo ameyasema wakati akiahirisha Bunge mjini Dodoma leo, na kusisitiza Serikali itahakikisha kuwa inawakamata wale wote ambao wamefanya mauji katika maeneo hayo kwani dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila raia wa Tanzania wakiwamo wananchi wa wilaya hiyo wanakua huru kufanya shughuli zao za maendeleo bila kuhofia usalama wa maisha yao.

Majliwa alisema serikali bado inaendelea kuchukua hatua za muda mfupi na muda mrefu kuhakikisha kuwa inarejesha hali ya usalama katika maeneo hayo, kwani wameongeza doria na vitendea kazi kwa askari pamoja na kuunda kanda maalumu ya kipolisi katika mkoa wa Pwani inayojumuisha maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

"Tayari kamanda wa polisi wa Kanda hiyo maalum amekwisha teuliwa, hivyo natoa wito kwa raia wema katika wilaya hizo waendelee kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuwezesha watuhumiwa wote kukamatwa" alisema Majaliwa.

Alisema kuwa hali ya ulinzi na usalama ni nzuri kwani usalama wa raia na mali zao unaendelea kulindwa na mipaka yote ya nchi ipo salama kutokana na vikosi vya ulinzi na usalama kuwa imara na madhubuti katika kulinda mipaka na usalama wa nchi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment