Writen by
sadataley
12:16 PM
-
0
Comments
Mbunge mmoja ambaye anaiunga mkono serikali ya Uganda aliyewasilisha hatua ya kuongeza muda wa rais kuhudumu na kupelekea malumbano ambapo wabunge wa upinzani waliondolewa kwa nguvu kutoka kwenye bunge.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP kuondolewa kwa wabunge hao kumekuja baada ya spika wa bunge mwanachama wa chama tawala alipowashutumu baadhi ya wabunge kwa kuvuruga utaratibu wa kikao cha Jumanne wakati wawakilishi walipowasilisha juhudi za kuelezea mswaada wa kuondoa umri wa rais wa miaka 75 kutoka kwenye katiba ya Uganda ili kuhudumu bila ya kuwepo kwa kipengele cha umri.
Picha kutoka kikao cha bunge zilionesha baadhi ya wabunge wa upinzani wakivutwa na kutolewa nje na wengine kuburuzwa na maafisa usalama ambao hawakuvaa sare za polisi. Kiongozi wa upinzani baada ya kulalamika kwamba kikosi maalumu kilitumiwa kuwatoa nje wabunge wenzake baadae aliongoza timu yake kutoka nje.
Hatua ya kuondoa kiwango cha umri imeonekana kama juhudi za Museveni kuongeza utawala wake. Rais Museveni amelikwepa swali iwapo ana nia ya kuwepo zaidi madarakani akisema hivi karibuni kwamba suala hilo sio muhimu. Lakini wakosoaji wanasema pembeni na mazungumzo hayo anaongoza hatua hiyo kwa wabunge kuondoa kipengele cha mwisho ili kuongeza muda wake wa urais ikiwezekana aongoze taifa hilo hadi kifo kitakapomkuta.Rais Yoweri Museveni ambaye ana umri wa miaka 73 na ametawala Uganda tangu alipochukua madaraka kwa nguvu mwaka 1986 hastahili kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 kama kipengele kinachozungumzia umri bado kitakuwepo ndani ya katiba ya Uganda. Rasimu ya mswaada lazima itangazwe katika gazeti la serikali kabla kujadiliwa katika bunge la taifa.
Kipengele cha rais kuhudumu kiliondolewa kutoka katika katiba ya Uganda ya mwaka 2005. Chama tawala nchini Uganda kinafurahia wingi wa wawakilishi wake katika bunge na mswaada unatarajiwa kupitishwa.
VOA Swahili
No comments
Post a Comment