Thursday, September 28, 2017

Wanawake wa Saudia wafurahia uwamuzi wa kuendesha gari

Azza Al Shmasani aingia ndani ya gari lake kukaidi marufuku ya kuendesha gari mjini Riyadh Azza Al Shmasani aingia ndani ya gari lake kukaidi marufuku ya kuendesha gari mjini Riyadh
Maoni yamegawika huko Saudi Arabia kufuatia uwamuzi wa Mfalme Salman kumruhusu mwanamke kuweza kuendesha gari kuanzia mwezi June Mwakani.
Wanaharakati waandishi habari na watumnishi wa umaa pamoja na wanawake wamefurahia uwamuzi huo wengi wakisema wa kihistoria na ushindi kwa harakati za wanawake kupata haki ya kujiamulia jinsi wanavyotaka kusafiri.
Abdallah Muawiya mwandishi habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Saudi Arabia, anasema wanaharakati waloanza mapambano yao tangu mwanzoni mwa miaka 1990 wamefurahia hatua hiyo.
"Kwa hiyo harakati zao hizi tunaweza kusema zimesaidia vile vile kuisukuma serikali mpaka Mfalme Salman kuweza kufikia uwamuzi huu wa kuwaruhusu kina mama kuendesha magari." amesema Muawiya.
Kamati maalum imeunda kuweka masharti na utaratibu kwa wanawake kuweza kupata liseni na kuruhusiwa kuendesha magari kuanzia mwezi June 2018.

VOA  Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment