Friday, September 29, 2017

Umoja wa Afrika wakosoa amri ya Rais Trump iliyo dhidi ya uhajiri

Kamisheni ya Umoja wa Afrika imekosoa vikali amri ya Rais Donald Trump wa Marekani ambayo iko dhidi ya wahajiri.
Rais Donald Trump wa Marekani
Kamisheni ya Umoja wa Afrika imetoa taarifa baada ya kikao chake na maafisa wa kijeshi wa kikosi cha pamoja cha nchi kadhaa cha kupambana na kundi la kigaidi la Boko Haram na kueleza kuwa, hatua ya Rais Donald Trump ya kuiongeza Chad katika orodha ya raia wanaopigwa marufuku kuingia nchini Marewkani si ya kiadilifu.
Taarifa ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika imeashiria nafasi ya Chad katika kupambana na ugaidi katikia ukanda wa Ziwa Chad, kaskazini mwa Mali na katika kikosi cha Sahel Afrika na kusisitiza kwamba,  kuwapiga marufuku raia wa Chad kuingia nchini Marekani ni hatua ambayo haihalalishiki.
Ikumbukwe kwamba katika kuhalalisha hatua yake ya kuitia Chad katika orodha ya nchi ambazo raia wake hawaruhusiwi kuinjgia nchini Marekani Rais Trump alidai kwamba, nchi hiyo haitoi ushirikiano wa ubadilishanaji taarifa na Washington katika suala la kupambana na ugaidi.
Itakumbukwa kuwa, katika uamuzi wake aliouchukua siku ya Jumatatu, Rais Donald Trump aliziongeza nchi za Korea Kaskazini, Chad na Venezuela katika orodha ya nchi ambazo raia wake hawaruhusiwi kufanya safari nchini Marekani. Nchi nyingine ni Iran, Syria, Libya, Somalia na Yemen. Aidha Sudan iliyokuwa katika orodha ya awali imeondolewa katika orodha mpya.
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment