Saturday, October 7, 2017

Obama: Diplomasia ni njia bora zaidi ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Peninsula ya Korea

Rais msataafu wa Marekani, Barack Obama amesema kuwa udiplomasia ndiyo njia bora zaidi ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Peninsula ya Korea na si nguvu ya kijeshi.
Obama amesema kuwa, kutilia mkazo suala la kutumiwa njia zisizo za kidiplomasia kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Peninsula ya Korea hakutafanikisha ufumbuzi wa suala hilo. Obama aliyasema hayo jana katika mkutano wa Kimataifa wa Universal Citizens huko Sao Paulo nchini Brazil uliohudhuriwa na wanaharakati wa kiuchumi 600 kutoka maeneo mbalimbali duniani.  
Rais Donald Trump wa Marekani katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akikosoa utendaji wa serikali ya Rais msatafu wa Marekani, Barack Obama huku akisitiza kutumiwa njia za kijeshi dhidi ya Korea ya Kaskazini ili kusitisha miradii ya makombora na nyuklia ya nchi hiyo. Hali ya mvutano katika Peninsula ya Korea ilishika kasi baada ya Korea ya Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora yake mawili ya balistiki yenye uwezo wa kuvuka mabara aina ya ICBM mwezi uliopita. 
Pyongyang inasisitiza kuwa itaendelea kuimarisha uwezo na nguvu zake za kijeshi madhali Marekani na waitifaki wake hususan Korea ya Kusini na Japan zinaendelea kufanya majaribio na kuitishia Korea ya Kaskazini.  
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment