Writen by
sadataley
10:17 AM
-
0
Comments
Mgeni rasmi katika maazimisho hayo
Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga
kwa kutimiza miaka 50 pamoja na kuzindua jarida maalum la kikosi hicho
akiwa amelishika linaitwa Uhodari.
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj
wakionyesha ukakamavu wake kwa kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la
kuburudisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya kikosi cha 841kj Baadhi ya
vijana waliopo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi maarufu kama
operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha 841kj mafinga nao
walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.
Hili ndio jengo linalojengwa kwa ajili
ya kiwanda cha Kukoboa na kusaga nafaka za kikosi cha jeshi la kujenga
taifa 841kj mafinga.
Na Fredy Mgunda,Mafinga
Kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj
mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao
wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo linajilisha na
kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.
Akizungumza kaimu kamanda wa kikosi cha
841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967 kikiwa na lengo la
kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John
Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga kiwanda
cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza
uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha ulinzi kutokana na
majukumu waliyonayo.
Nkya alisema kuwa kikosi cha 841kj kj
mafinga kimeamua kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa kinaendeshwa
kibiashara ili kukuza ajira na pato la taifa.
“Hapa kikosini tunalima na kufuga mifugo
ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa kiwango kinachotakiwa kukidhi soko
ili kuonyesha kuwa kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga
kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja ya kuanzishwa kwa kikosi
hicho”.alisema Nkya
Captain Nkya alisema Sasa hivi Jeshi la
kujenga taifa kikosi cha 841kj kimekuwa kikosi cha Kisasa nachenye
wasomi wengi wanaweza kusaidia kubuni vitu vingi vyenye faida ya
kulisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za
kijamii.
“Tumefungua kiwanda ni lazima sasa
kuongeza uzalishaji kwa lengo la kuja kuipunguzia serikali gharama za
kukihudumia kikosi cha 841kj mafinga ukiangalia tunaeneo kubwa na
tunanguvu kazi hivyo ni lazima tulime na kufuga kwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli anataka jeshi la kujenga
taifa lirudi kujitegemea”.alisema Nkya
Kwa upande wake mgeni rasmi katika
maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha
841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 kwa kuwa kudumu huko kwa kikosi
hicho ni hatua kubwa sana katika ujenzi wa taifa.
Chale alikitaka kikosi cha 841kj
kurudisha uzalendo kama zamani ili kuendelea kuzalisha chakula kwa wingi
kama zamani kwa saizi kikosi hicho kinalima eneo dogo sana kitu
kinachochangia kuipa serikali wakati mgumu wa kikihudumia kikosi hicho.
“Nimetembea eneo kubwa sana leo lakini
nimeona eneo la uzalishaji ni dogo sana hivyo mnahitaji kuongeza
uzalishaji ili kuisadia serikali kuzalisha chakula kwa wingi nyie mna
nguvu kazi hapa lakini bado sijaona mkiitumia ipasavyo”.alisema Chale
Aidha Chale alikipongezakikosi hicho cha
841kj mafinga kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuanza ujenzi wa kiwanda ambacho
kitaongeza ajira,uzalishaji wa bidhaa za chakula na kukuza uchumi wa
nchi kutokana na uzalishaji wake.
“Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa
kuweza kuwa na wazo zuri kama hili la kujenga kiwanda hapo ndio mnakuwa
mnatimiza malengo ya kikosi cha 841kj mafinga kwa kukuza uzalishaji kwa
kutumia raslimali watu ambao mnao katika kiosi kuzalisha na sio kila
siku mnakuwa mnategemea msaada kutoka serikalini”alisma Chale
Chale alikitaka kikosi kuendelea kutunza
nidhamu waliyonayo na kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli katika jitihada zake za
kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi na viwanda.
Naye Bwana shamba wakikosi (farm
manager) luteni Francis Breek wa kikosi cha 841kj alisema kuwa
wamejipanga kuongeza uzalishaji kwa kuwa wana eneo kubwa na wana
wataalamu wengi wanaoweza kukidhi mahitaji ya kukuza uzalishaji.
“Ukiangalia mwaka huu tumelima eneo
kubwa na tumeongeza idadi ya mifugo hivyo tunatarajia kuongeza tena
idadi ya mifugo na kupanua eneo la kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa
kuwa tumejenga kiwanda na kiwanda kinahitaji uzalishaji mkubwa wa nafaka
pamoja na ufugaji mkubwa na wenye tija”alisema Breek
Lakini pia kikosi hicho cha 841kj
Mafinga kilizindua jarida linaloitwa uhodari ambalo linaonesha kila kitu
kinachofanywa na kilichofanywa na kikosi hichotoka kuanzishwa kwake.
“Hongera kikosi cha 841kj kwa Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa kwake”
Chanzo:Mjengwa Blog
No comments
Post a Comment