Sunday, July 9, 2017

Tume ya Uchaguzil: Uchaguzi DRC hauwezi kufanyika Disemba mwaka huu

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Corneille Nangaa Yobeluo 
Rais Joseph Kabila
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Corneille Nangaa Yobeluo amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu nchini humo hauwezi kufanyika mwezi Desemba au kabla ya mwezi huo mwaka huu kama ilivyopangwa kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza jijini Paris, Ufaransa Corneille Nangaa amesema kuwa, sababu kubwa inayofanya uchaguzi huo kutofanyika kama ilivyopangwa ni kukosekana amani na usalama katika jimbo la Kasai.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, jitihada zinafanyika kuhakikisha kuwa wakaazi wa kasai wanasajiliwa kama wapiga kura kuanzia mwezi ujao wa Agosti.
Kwa mujibu wa mkataba wa kisiasa uliofikiwa mwezi Desemba mwaka uliopita, ilikubaliwa kuwa uchaguzi katika nchi hiyo ufanyike mwezi Disemba na Rais Joseph Kabila kutowania
Rais Kabila mwenyewe amekuwa akisema kuwa, uchaguzi utafanyika nchini humo lakini hajawahi kusema utafanyika lini.
Wanasiasa wa upinzani nchini humo wamekuwa wakisema kuwa Rais Kabila anachelewesha makusudi mchakato wa maandalizi ya uchaguzi ili kuendelea kubakia madarakani.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiitaka Tume ya Uchaguzi nchini humo kutangaza kalenda ya Uchaguzi, na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika mwaka huu kama ilivyopangwa.
Eneo la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekumbwa na machafuko ya umwagaji damu tangu mwezi Septemba 2016 na tangu wakati huo hadi hivi sasa, vikosi vya serikali vinapambana na kundi moja la waasi lililozuka kwenye eneo hilo.
Pastoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment